Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 28:13-20

Methali 28:13-20 BHN

Afichaye makosa yake hatafanikiwa; lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema. Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima; lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa. Mtawala mwovu anayewatawala maskini, ni kama simba angurumaye au dubu anayeshambulia. Mtawala asiye na akili ni mdhalimu mkatili; lakini achukiaye mali ya udanganyifu atatawala muda mrefu. Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu, atakuwa mkimbizi mpaka kaburini; mtu yeyote na asijaribu kumzuia. Aishiye kwa unyofu atasalimishwa, lakini mdanganyifu ataanguka kabisa. Anayelima shamba lake atapata chakula kingi, bali anayefuata yasiyofaa atapata umaskini tele. Mtu mwaminifu atapata baraka tele, lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu.

Soma Methali 28

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Methali 28:13-20