Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 17:17-28

Methali 17:17-28 BHN

Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu. Si jambo la akili kuweka rehani, na kuwa mdhamini wa mtu mwingine. Anayependa ugomvi anapenda dhambi; anayejigamba anajitafutia maangamizi. Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi, na msema uongo hupatwa na maafa. Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake, na baba wa mpumbavu hana furaha. Moyo mchangamfu ni dawa, bali moyo wenye huzuni hudhoofisha mwili. Mtu mbaya hupokea hongo kwa siri ili apate kupotosha haki. Mtu mwenye busara lengo lake ni hekima, lakini mpumbavu hupania kila kitu duniani. Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake, na uchungu kwa mama yake mzazi. Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia; ni kosa kumchapa viboko muungwana. Asiyesema sana ana maarifa; mtu mtulivu ni mwenye busara. Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima; akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.

Soma Methali 17