Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 2:23-27

Wafilipi 2:23-27 BHN

Kwa hiyo natumaini kumtuma kwenu mara nitakapojua jinsi mambo yatakavyoniendea. Na, ninatumaini katika Bwana kwamba nami pia nitaweza kuja kwenu karibuni. Nimeona sina budi kumtuma kwenu ndugu yetu Epafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini na vitani na ambaye ni mjumbe wenu aliyenisaidia katika mahitaji yangu. Anayo hamu kubwa ya kuwaoneni nyinyi nyote, na amesikitika sana kwani nyinyi mmepata habari kwamba alikuwa mgonjwa. Naam, alikuwa mgonjwa hata karibu ya kufa. Lakini Mungu alimwonea huruma, na si yeye peke yake, ila na mimi pia ili nisipate uchungu zaidi.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Wafilipi 2:23-27