Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 27:3-10

Mathayo 27:3-10 BHN

Hapo, Yuda, ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu vile vipande thelathini vya fedha. Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.” Naye akazitupa zile fedha hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga. Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya hekalu kwa maana ni fedha za damu.” Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni. Ndio maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu. Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: “Walichukua vipande thelathini vya fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walimtia bei, wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 27:3-10