Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 26:31-35

Mathayo 26:31-35 BHN

Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu wa leo, nyinyi nyote mtakuwa na mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema: ‘Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.’ Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni Galilaya.” Petro akamwambia Yesu, “Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe.” Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Petro akamwambia, “Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Wale wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.