Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 16:15-19

Mathayo 16:15-19 BHN

Yesu akawauliza, “Na nyinyi je, mnasema mimi ni nani?” Simoni Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Yesu akasema, “Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana hakuna binadamu yeyote aliyekufunulia jambo hili, ila Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia: Wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda. Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mbinguni.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 16:15-19