Mathayo 16:13-20
Mathayo 16:13-20 BHN
Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasema Mwana wa Mtu kuwa ni nani?” Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane Mbatizaji, wengine Elia, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.” Yesu akawauliza, “Na nyinyi je, mnasema mimi ni nani?” Simoni Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Yesu akasema, “Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana hakuna binadamu yeyote aliyekufunulia jambo hili, ila Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia: Wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda. Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mbinguni.” Kisha akawaonya wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo.