Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kidogo cha Maombolezo ni mkusanyiko wa tenzi tano, ambamo mwandishi anaomboleza juu ya kuteketezwa kwa Yerusalemu mwaka 586 K.K. Anamnung'unikia Mungu juu ya tukio hilo lakini watu wa Israeli na viongozi wao ndio hasa waliosababisha kuharibiwa kwa Yerusalemu, na wao ndio wanaolaumiwa. Hata hivyo katika maombolezo hayo, watu wanatiwa moyo na kupewa tumaini kwamba Mungu atawasaidia siku za usoni.
Katika ibada za Wayahudi tenzi hizo zilitumiwa wakati wa adhimisho la mfungo wa kila mwaka ambapo walikumbuka kuharibiwa kwa hekalu la kwanza huko Yerusalemu.
Tenzi nne za kwanza katika Kiebrania zimeandikwa kwa kufuata mfumo wa alfabeti 22 za Kiebrania. Kutokana na mpangilio huo, sura 1, 2 na 4 zina aya 22, hali sura ya 3 ina aya 66. Lakini ni jambo la kushangaza pia kwamba sura ya 5 nayo ina aya 22 lakini hazikuandikwa katika mtindo huo wa kuanzia na alfabeti hizo.

Iliyochaguliwa sasa

Maombolezo Utangulizi: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia