Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 2:1-10

Yona 2:1-10 BHN

Basi, Yona, akiwa tumboni mwa samaki huyo, akawa akimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akisema: “Kwa sababu ya taabu yangu, nilikuomba, ee Mwenyezi-Mungu, nawe ukanisikiliza; toka chini kuzimu, nilikulilia, nawe ukasikiliza kilio changu. Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari, gharika ikanizunguka, mawimbi na gharika vikapita juu yangu. Nilidhani kwamba nimetengwa nisiwe mbele yako; nisiweze kuliona tena hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka na kunisonga; kilindi kilinifikia kila upande, majani ya baharini yakanifunika kichwa. Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni. Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, sala yangu ikakufikia, katika hekalu lako takatifu. Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili, huutupilia mbali uaminifu wao kwako. Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea sadaka, na kutimiza nadhiri zangu. Mwenyezi-Mungu, ndiye aokoaye.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona kwenye nchi kavu.

Soma Yona 2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha