Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 6

6
1Yobu akamjibu Elifazi:
2“Laiti mahangaiko yangu yangepimwa uzani wake,
mateso yangu yote yakawekwa katika mizani!
3Yangekuwa mazito kuliko mchanga wa pwani.
Ndio maana maneno yangu ni ya kuropoka!
4Naam, mishale ya Mungu Mwenye Nguvu imenichoma;
nafsi yangu imekunywa sumu yake.
Vitisho vya Mungu vimenikabili.
5Je, pundamwitu hulia akiwa na majani,
au ng'ombe akiwa na malisho?
6Je, kitu kisicho na ladha chaweza kuliwa bila chumvi?
Je ute wa yai una utamu wowote?
7Sina hamu ya kuvigusa vyakula hivyo,
hivyo ni vyakula vyangu vichukizavyo.#6:7 Sehemu ya pili ya aya katika Kiebrania si dhahiri na tafsiri yake hapa si hakika.”
8“Laiti ningejaliwa ombi langu,
Mungu akanipatia kile ninachotamani:
9Kwamba angekuwa radhi kunipondaponda,
angenyosha mkono wake anikatilie mbali!
10Hiyo ingekuwa faraja yangu,
ningefurahi#6:10 ningefurahi: Maana katika Kiebrania si dhahiri. katika maumivu yasiyo na huruma.
11Lakini sina nguvu ya kuweza kuendelea;
sijui mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia.
12Je, nguvu zangu ni kama za mawe?
Au mwili wangu kama shaba?
13Kweli kwangu hamna cha kunisaidia;
msaada wowote umeondolewa kwangu.
14“Anayekataa#6:14 Anayekataa: Maana katika Kiebrania si dhahiri. kumhurumia rafiki yake,
anakataa kumcha Mungu mwenye nguvu.
15Rafiki zangu wamenidanganya kama kijito,
wamenihadaa kama mitaro isiyo na maji.
16Ambayo imejaa barafu,
na theluji imejificha ndani yake.
17Lakini wakati wa joto hutoweka,
wakati wa hari hubaki mito mikavu.
18Misafara hupotea njia wakitafuta maji,
hupanda nyikani na kufia huko.
19Misafara ya Tema hutafuta tafuta,
wasafiri wa Sheba hutumaini.
20Huchukizwa kwa kutumaini bure,
hufika kwenye vijito hivyo na kuudhika.
21Nyinyi mmekuwa kama vijito hivyo,
mwaona balaa yangu na kuogopa.
22Je, nimesema mnipe zawadi?
Au mnitolee rushwa kwa mali zenu?
23Au mniokoe makuchani mwa adui?
Au mnikomboe mkononi mwa wadhalimu?
24“Nifundisheni, nami nitanyamaza.
Nielewesheni jinsi nilivyokosea.
25Maneno ya kweli yana nguvu kubwa!
Lakini makaripio yenu yananikosoa nini?
26Je, mnadhani kwamba mwaweza kuyakosoa maneno?
Maneno ya mtu aliyekata tamaa ni upepo tu.
27Nyinyi mnathubutu hata kuwapigia yatima kura;
mnawapigia bei hata marafiki zenu!
28Lakini sasa niangalieni tafadhali.
Mimi sitasema uongo mbele yenu.
29Acheni tafadhali, kusiwe na uovu;
acheni sasa, kwani mimi ni mnyofu.
30Je, mnadhani kwamba nimesema uovu?
Je, mnafikiri mimi siyatambui machungu?

Iliyochaguliwa sasa

Yobu 6: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia