Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 30:17-22

Yeremia 30:17-22 BHN

“Nitakurudishia afya yako, na madonda yako nitayaponya, japo wamekuita ‘Aliyetupwa’, ‘Mji Siyoni usio na wa kuutunza!’” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitazirudisha tena fanaka za maskani ya Yakobo, na kuyaonea huruma makao yake; mji utajengwa upya juu ya magofu yake, na ikulu ya mfalme itasimama pale ilipokuwa. Humo zitatoka nyimbo za shukrani na sauti za wale wanaosherehekea. Nitawaongeza na wala hawatakuwa wachache; nitawafanya waheshimiwe wala hawatadharauliwa. Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani, jumuiya yao itaimarika mbele yangu, nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza. Kiongozi wao atakuwa mmoja wao, mtawala wao atatokea miongoni mwao. Nitamleta karibu naye atanikaribia; maana, nani anayethubutu kunikaribia kwa nguvu zake? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”

Soma Yeremia 30