Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 9:2-6

Isaya 9:2-6 BHN

Watu waliotembea gizani wameona mwanga mkubwa. Watu walioishi katika nchi ya giza kuu, sasa mwanga umewaangazia. Wewe, ee Mungu, umelikuza taifa, umeiongeza furaha yake. Watu wanafurahi mbele yako, wana furaha kama wakati wa mavuno, kama wafurahivyo wanaogawana nyara. Maana nira nzito walizobeba, nira walizokuwa wamefungwa, na fimbo ya wanyapara wao, umezivunjavunja kama wakati wa Wamidiani. Viatu vyote vya washambulizi vitani na mavazi yote yenye madoa ya damu yatateketezwa kama kuni za kuwasha moto. Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu, tumepewa mtoto wa kiume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa: “Mshauri wa Ajabu”. “Mungu Mwenye Nguvu”, “Baba wa Milele”, “Mfalme wa Amani”.

Soma Isaya 9

Verse Image for Isaya 9:2-6

Isaya 9:2-6 - Watu waliotembea gizani
wameona mwanga mkubwa.
Watu walioishi katika nchi ya giza kuu,
sasa mwanga umewaangazia.
Wewe, ee Mungu, umelikuza taifa,
umeiongeza furaha yake.
Watu wanafurahi mbele yako,
wana furaha kama wakati wa mavuno,
kama wafurahivyo wanaogawana nyara.
Maana nira nzito walizobeba,
nira walizokuwa wamefungwa,
na fimbo ya wanyapara wao,
umezivunjavunja kama wakati wa Wamidiani.
Viatu vyote vya washambulizi vitani
na mavazi yote yenye madoa ya damu
yatateketezwa kama kuni za kuwasha moto.
Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu,
tumepewa mtoto wa kiume.
Naye atapewa mamlaka ya kutawala.
Ataitwa: “Mshauri wa Ajabu”.
“Mungu Mwenye Nguvu”,
“Baba wa Milele”,
“Mfalme wa Amani”.