Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 50:4-8

Isaya 50:4-8 BHN

Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza. Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao. Bwana Mungu hunisaidia, kwa hiyo siwezi kufadhaika. Uso wangu nimeukaza kama jiwe; najua kwamba sitaaibishwa. Mtetezi wangu yuko karibu. Ni nani atakayepingana nami? Na aje tusimame mahakamani. Adui yangu ni nani? Na ajitokeze mbele basi.

Soma Isaya 50