Isaya 40:6-8
Isaya 40:6-8 BHN
Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!” Nami nikauliza, “Nitangaze nini?” Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani; uthabiti wao ni kama ua la shambani. Majani hunyauka na ua hufifia, Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake. Hakika binadamu ni kama majani. Majani hunyauka na ua hufifia, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”