Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 33:17-24

Isaya 33:17-24 BHN

Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake, mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana. Mtafikiria tisho lililopita na kujiuliza, “Wako wapi wale waliokadiria na kukisia kodi? Wako wapi wale waliopeleleza ulinzi wetu?” Hamtawaona tena watu wale wenye kiburi, wanaozungumza lugha isiyoeleweka. Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu; tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara; vigingi vyake havitangolewa kamwe, kamba zake hazitakatwa hata moja. Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake. Kutakuwa na mito mikubwa na vijito, ambamo meli za vita hazitapita, wala meli kubwa kuingia. Maana Mwenyezi-Mungu ni hakimu wetu, yeye ni mtawala wetu; Mwenyezi-Mungu ni mfalme wetu, yeye ndiye anayetuokoa. Ewe Siyoni, kamba zako zimelegea, haziwezi kushikilia matanga yake, wala kuyatandaza. Lakini nyara nyingi zitagawanywa; hata vilema wataweza kuchukua sehemu yao. Hakuna atakayesema tena ni mgonjwa; watu watasamehewa uovu wao wote.

Soma Isaya 33