Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 25

25
Wimbo wa sifa kwa Mungu
1Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe Mungu wangu;
nitakutukuza na kulisifu jina lako,
kwa maana umetenda mambo ya ajabu;
waitekeleza kwa uaminifu na kweli
mipango uliyoipanga tangu zamani.
2Umeufanya mji ule kuwa rundo la mawe,
mji wenye ngome kuwa uharibifu.
Majumba ya watu wageni yametoweka,
wala hayatajengwa tena upya.
3Kwa hiyo watu wenye nguvu watakutukuza,
miji ya mataifa katili itakuogopa.
4Maana wewe umekuwa ngome kwa maskini,
ngome kwa fukara katika taabu zao.
Wewe ni kimbilio wakati wa tufani,
kivuli wakati wa joto kali.
Kweli pigo la watu wakatili ni kali
kama tufani inayopiga ukuta;
5ni kama joto la jua juu ya nchi kavu.
Lakini wewe wakomesha fujo ya wageni.
Kama wingu lizimavyo joto la jua
ndivyo ukomeshavyo nyumba za ushindi za wakatili.
6Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi. 7Katika mlima huuhuu, Mwenyezi-Mungu ataliondoa wingu la huzuni lililowafunika watu wote, kifuniko cha uchungu juu ya mataifa yote. 8#25:8 Taz 1Kor 15:54; Ufu 7:17; 21:4 Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote. Bwana Mwenyezi-Mungu ametamka.
9Siku ile, watu wote watasema, “Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemngojea atuokoe. Huyu ndiye Mwenyezi-Mungu tuliyemtazamia. Njoni tufurahi na kushangilia kwa kuwa ametuokoa.”
Mungu ataiadhibu Moabu
10 #25:10-12 Taz Isa 15:1--16:14; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11; Amo 2:1-3; Sef 2:8-11 Mwenyezi-Mungu ataulinda mlima wa Siyoni, lakini watu wa Moabu watakanyagwakanyagwa nchini mwao kama nyasi katika shimo la mbolea. 11Watainyosha mikono yao kama mtu anayejaribu kuogelea, lakini pamoja na ustadi wao, Mwenyezi-Mungu ataporomosha kiburi chao. 12Atayabomoa maboma ya miji ya Moabu yenye kuta ndefu na kuyabwaga chini mavumbini.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 25: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha