Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 20:2-4

Isaya 20:2-4 BHN

Miaka mitatu kabla ya hapo, Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwambia Isaya, mwana wa Amozi hivi: “Nenda ukavue vazi la gunia unalovaa kiunoni, na viatu miguuni mwako.” Isaya akafanya hivyo; akawa anatembea uchi na bila viatu. Basi, mnamo mwaka huo mji wa Ashdodi ulipotekwa, Mwenyezi-Mungu alisema: “Mtumishi wangu Isaya amekuwa akitembea uchi na bila viatu kwa muda wa miaka mitatu sasa, kama ishara na alama dhidi ya nchi ya Misri na Kushi. Basi, mfalme wa Ashuru atawachukua mateka Wamisri na Wakushi, wakubwa kwa wadogo. Watachukuliwa, nao watatembea uchi na bila viatu; matako wazi, kwa aibu ya Misri.

Soma Isaya 20