Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 15

15
Mungu ataiangamiza Moabu
1 #15:1--16:14 Taz Isa 25:10-12; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11; Amosi 2;1-3; Sef 2:8-11 Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Moabu.
Mji wa Ari nchini Moabu umeangamizwa usiku;
mji wa Kiri#15:1 Ari, Kiri: Hiyo ilikuwa miji mikubwa nchini Moabu. nchini Moabu umeteketezwa usiku.
2Watu wa Diboni wamepanda hekaluni, hadi mahali pa juu kuomboleza,
watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba;
vichwa vyote vimenyolewa upara,
ndevu zao zote zimekatwa kabisa.
3Wanapita njiani wamevaa mavazi ya gunia.
Kwenye paa za nyumba na viwanja vya mji
watu wanalia na kukauka kwa machozi.
4Watu wa Heshboni na Eleale wanalia,
sauti zao zinasikika hadi Yahazi.
Hata askari wa Moabu wanalia kwa sauti;
mioyo yao inatetemeka.
5Moyo wangu unasononeka juu ya nchi ya Moabu;
wakimbizi wake wanakimbilia Soari,
wanakimbia mpaka Eglath-shelishiya.
Wanapanda njia ya kwenda Luhithi wakilia,
njiani kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
6Kijito cha Nimrimu kimekauka;
nyasi zimekauka, majani mabichi yamenyauka,
hakuna chochote kinachoota hapo.
7Watu wanavuka kijito cha Mierebi
wamebeba mali yao yote waliyochuma,
na kila walichojiwekea kama akiba.
8Kilio kimezuka pote nchini Moabu,
maombolezo yao yamefika Eglaimu,
naam, yamefika mpaka Beer-elimu.
9Maji ya Diboni yamejaa damu,
lakini Mungu ataongeza msiba wa Diboni.
Hao wachache watakaobaki hai
na kukimbia kutoka nchini Moabu,
watapelekewa simba wa kuwaua.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 15: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia