Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Habakuki 3:16-19

Habakuki 3:16-19 BHN

Nasikia hayo nami ninashtuka mwilini, midomo yangu inatetemeka kwa hofu; mifupa yangu inateguka, miguu yangu inatetemeka. Ninangojea kwa utulivu siku ile ya maafa, ambayo inawajia wale wanaotushambulia. Hata kama mitini isipochanua maua, wala mizabibu kuzaa zabibu; hata kama mizeituni isipozaa zeituni, na mashamba yasipotoa chakula; hata kama kondoo wakitoweka zizini, na mifugo kukosekana mazizini, mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi-Mungu nitamshangilia Mungu anayeniokoa. Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani.

Soma Habakuki 3