Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 21:1-7

Mwanzo 21:1-7 BHN

Mwenyezi-Mungu alimkumbuka Sara, akamtendea kama alivyoahidi. Basi, Abrahamu akiwa mzee, Sara akapata mimba, akamzalia mtoto wa kiume, wakati uleule Mungu alioutaja. Abrahamu akampa huyo mwanawe ambaye Sara alimzalia jina Isaka. Isaka alipotimiza umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri kama alivyoamriwa na Mungu. Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 100 wakati mwanawe Isaka alipozaliwa. Naye Sara akasema, “Mungu amenipatia kicheko; yeyote atakayesikia habari hizi, atacheka pamoja nami.” Kisha akaongeza, “Ni nani angeweza kumwambia Abrahamu kwamba mimi Sara nitanyonyesha watoto? Tena nimemzalia mtoto wa kiume katika uzee wake!”

Soma Mwanzo 21

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 21:1-7

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha