Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Esta UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Esta kinasimulia jinsi jumuiya moja ya Kiyahudi ilivyookolewa kutoka vitisho vya kuangamizwa. Mambo hayo yalitokea huko mjini Susa wakati utawala wa Persia ulipokuwa umeenea katika Mashariki ya Kati yote mpaka Misri. Baadhi ya jamaa maarufu za watu wa Israeli hawakurejea makwao kutoka Babuloni wakati wa kuangamia kwa utawala wa Babuloni (mwaka 539 K.K.). Watu hao walikumbana mara kwa mara na uadui kutoka kwa wenyeji wa huko, kwani Wayahudi aghalabu walikuwa wanafuata sheria na desturi zao zilizokuwa tofauti sana na za watu wengine.
Esta alikuwa msichana Myahudi ambaye alikuwa malkia wa Persia. Yeye pamoja na Mordekai ambaye alikuwa baba mlezi wake walijua hizo njama za kuwaua Wayahudi.
Kwa kutueleza uhasama uliozuka kati ya Mordekai na Hamani, waziri mkuu wa mfalme Artashasta, na jinsi Esta pamoja na Mordekai walivyofaulu kuondolea mbali tishio la kuwaangamiza Wayahudi, simulizi la kitabu hiki lina shabaha ya kueleza chanzo na asili ya sikukuu moja maarufu ya Wayahudi iitwayo Purimu ambayo huadhimishwa kabla ya Pasaka.

Iliyochaguliwa sasa

Esta UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia