Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso 5:8-14

Waefeso 5:8-14 BHN

Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga, maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana. Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni. Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. Lakini kila kitu kikifichuliwa na mwanga, ukweli wake hudhihirishwa; na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: “Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangaza.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waefeso 5:8-14