Amosi 5:10-17
Amosi 5:10-17 BHN
Nyinyi huwachukia watetezi wa haki na wenye kusema ukweli mahakamani. Nyinyi mnawakandamiza fukara na kuwatoza kodi ya ngano kupita kiasi. Mnajijengea nyumba za mawe ya kuchonga, lakini nyinyi hamtaishi humo; mnalima bustani nzuri za mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake. Maana mimi najua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu; nyinyi mnawatesa watu wema, mnapokea rushwa na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani. Basi, kutakuwa na wakati mbaya ambao hata mwenye busara atanyamaza. Tafuteni kutenda mema na si mabaya, ili nyinyi mpate kuishi naye Mwenyezi-Mungu wa majeshi awe pamoja nanyi kama mnavyosema. Chukieni uovu, pendeni wema, na kudumisha haki mahakamani. Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki. Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga. Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu; maana nitapita kati yenu kuwaadhibu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.”