Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 16:14-15

Matendo 16:14-15 BHN

Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema. Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika akisema, “Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni nyumbani kwangu mkakae.” Akatuhimiza twende.

Video for Matendo 16:14-15

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Matendo 16:14-15