3 Yohane 1:11-14
3 Yohane 1:11-14 BHN
Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu. Kila mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoa ushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni kweli. Ninayo bado mengi ya kukuambia, lakini sipendi kuyaandika kwa kalamu na wino. Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.