Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 20

20
Daudi anauteka mji wa Raba
(2Sam 12:26-31)
1Hata ikawa katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi na kuteka nyara nchi ya Waamoni, pia akaenda na kuuzingira Raba. Lakini Daudi alibaki huko Yerusalemu. Naye Yoabu aliushambulia Raba na kuuharibu; 2naye Daudi akaichukua taji ya mungu wao Milkomu kichwani pake; naye aligundua ya kwamba taji hiyo ilikuwa na uzito wa kilo thelathini na tano za dhahabu na ndani yake mlikuwemo kito cha thamani. Naye Daudi akakitwaa kupambia taji yake. Pia, aliteka idadi kubwa ya nyara kutoka katika mji huo. 3Halafu aliwachukua watu wa mji huo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sururu za chuma na mashoka ya chuma. Hivyo ndivyo alivyoitenda miji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.
Vita na majitu ya Wafilisti
(2Sam 21:15-22)
4Baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri. Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai aliyekuwa mmojawapo wa wazawa wa Warefai;#20:4 wazawa wa majitu: Kiebrania: Warefai. hivyo Wafilisti wakawa wameshindwa.
5Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.
6Baadaye kulitokea tena vita huko Gathi ambako kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na kimo kikubwa, na vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake vidole ishirini na vinne. Yeye pia alikuwa mzawa wa majitu. 7Naye alipowatukana Waisraeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, alimuua. 8Hao walikuwa wazawa wa majitu huko Gathi; nao waliuawa na Daudi pamoja na watumishi wake.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 20: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia