Ezra UTANGULIZI
UTANGULIZI
Vitabu vya Mambo ya Nyakati, hiki cha Ezra, pamoja na kitabu kinachofuata cha Nehemia, vyote vimetokana na mazingira yaleyale. Kitabu hiki kimepewa jina la mtu maarufu aitwaye Ezra ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa Wayahudi wakati waliporudi kutoka uhamishoni.
Kitabu chenyewe chaanza na tangazo rasmi lililotolewa na mfalme Koreshi wa Persia kuwaruhusu watu wa Israeli warejee makwao kujenga upya hekalu la Yerusalemu (sura 1). Kisha tunapewa idadi kubwa ya hao wakimbizi ambao walianza safari ya kurudi makwao (sura 2). Shughuli yao ya kwanza huko Yerusalemu ilikuwa kupata ile madhabahu ya dhabihu na kuanzisha tena ibada kwa Mungu (sura 3). Matayarisho hayo hata hivyo yalisababisha upinzani kutoka kwa maadui na kwa sababu hiyo kukawa na barua kadha wa kadha kwa wakuu wa Persia ambao walithibitisha kwamba idhini ilikuwa imekwisha tolewa (sura 4–6).
Sehemu ya pili ya kitabu inaeleza jinsi kuhani Ezra, akiwa ametumwa na mfalme Artashasta, alivyofufua na kurekebisha maisha ya dini huko Yerusalemu (sura 7–10).
Ujumbe wa kitabu cha Ezra unasisitiza na kutilia mkazo umuhimu wa imani na maisha mema na safi.
Iliyochaguliwa sasa
Ezra UTANGULIZI: BHND
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Jifunze Mengi Kuhusu Biblia Habari Njema