Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 7

7
Noa anaingia chomboni.
1Bwana akamwambia Noa: Ingia chomboni wewe na mlango wako wote! Kwani nimekuona kuwa mwongofu machoni pangu katika kizazi hiki. 2Namo miongoni mwao nyama wote wa nyumbani wanaotakata jichukulie saba saba, mume na mkewe, nao nyama wa nyumbani wasiotakata chukua wawili wawili tu, mume na mkewe!#1 Mose 8:20; 3 Mose 11. 3Nao ndege wa angani chukua saba saba wa kiume na wa kike, niwaponye wa kuzaa katika nchi yote nzima. 4Kwani ziko bado siku saba, ndipo, mimi nitakaponyesha mvua siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, niwatoweshe katika nchi yote nzima wote pia wanaosimama bado, niliowaumba mimi. 5Noa akayafanya yote, kama Bwana alivyomwagiza.#1 Mose 6:22. 6Naye Noa alikuwa mwenye miaka 600 hapo, mafuriko ya maji mengi yalipokuwa juu ya nchi.
7Noa akaingia chomboni pamoja na wanawe na mkewe na wake wa wanawe, mafuriko ya maji yalipokuw hayajawa bado.#1 Petr. 3:20. 8Nao nyama wanaotakata nao wasiotakata nao ndege nao wote wanaotambaa katika nchi, 9wakaingia wawili wawili chomboni mwake Noa, wa kiume na wa kike, kama Mungu alivyomwagiza Noa.#1 Mose 6:19. 10Ikawa, zile siku saba zilipokwisha pita, mafuriko ya maji yakawa juu ya nchi.
Mafuriko ya maji.
11Katika mwaka wa 600 wa siku zake Noa katika mwezi wa pili siku ya kumi na saba ya mwezi siku hiyo ndipo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipobubujika, nayo madirisha ya mbinguni yakafunguliwa, 12mvua ikanyesha katika nchi siku 40 mchana kutwa na usiku kucha. 13Siku ileile Noa akaingia chomboni, na Semu na Hamu na Yafeti, wanawe Noa, na mkewe Noa, nao wake watatu wa wanawe pamoja nao. 14Tena pamoja nao nyama wote wa porini wa kila namna nao nyama wote wa nyumbani wa kila namna na wadudu wote wanaotambaa katika nchi wa kila namna na wote walioweza kuruka wa kila namna na ndege wote nao wote wenye mabawa; 15wakaingia chomboni kwake Noa wawili wawili miongoni mwao wote wenye miili walio na pumzi za uzima. 16Miongoni mwao hao wote wenye miili wakaja mume na mke, wakaingia kwake, kama Mungu alivyomwagiza. Kisha Bwana akamfungia.
17Basi, yakawako mafuriko ya maji siku 40 juu ya nchi; maji yalipokuwa mengi yakakieleza kile chombo, kikawa juu ya nchi. 18Hayo maji yakakaza kuwa yenye nguvu, yakawa mengi sana juu ya nchi, nacho kile chombo kikaelea juu ya maji. 19Hayo maji yalipokaza kuwa yenye nguvu yakapanda, yakapanda juu ya nchi, mpaka ikifunikizwa milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu; 20hayo maji yakaipita juu mikono 15; ndivyo, milima ilivyofunikizwa. 21Ndipo, walipokufa wote wenye miili wao waliotembea katika nchi: ndege na nyama wa nyumbani na nyama wa porini na wadudu wote waliotambaa katika nchi, nao watu wote.#Iy. 22:15-16; 2 Petr. 3:6. 22Wote pia waliovuta puani mwao pumzi za roho yenye uzima, miongoni mwao wote waliokaa pakavu wakafa. 23Ndivyo, alivyowatowesha wote waliosimama juu ya nchi kuanzia watu, tena nyama na wadudu nao ndege wa angani, walitoweshwa wote katika nchi, akasalia Noa peke yake pamoja nao waliokuwa naye mle chomboni. 24Nayo hayo maji yakakaza kuwa yenye nguvu zizo hizo juu ya nchi siku 150.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 7: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia