Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 18

18
Mungu anamtokea Aburahamu tena.
1Kisha Bwana akamtokea katika kimwitu cha Mamure, mwenyewe alipokuwa amekaa hapo pa kuingia hemani kwa kuwa jua kali. 2Alipoyainua macho yake akaona watu watatu, wakisimama hapo, alipo; alipowaona akawapigia mbio na kuondoka hapo pa kuingia hemani, akawainamia chini,#Ebr. 13:2. 3akawaambia: Bwana wangu, kama nimeona mapendeleo machoni pako, usipite penye mtumishi wako! 4Mtaletewa maji kidogo ya kuiosha miguu yenu, kisha mtapumzika chini ya mti huu. 5Nami nitaleta chakula kidogo, mioyo yenu ipate kutulia, kisha mtakwenda zenu, kwani huku, mnakopita, ni kwake mtuma wenu. Nao wakamwambia: Fanya, kama ulivyosema! 6Aburahamu akaingia upesi hemani kwa Sara, akamwambia: Chukua upesi pishi sita za unga mwembamba uliochungwa vema, uukande, utengeneze mikate! 7Kisha Aburahamu akapiga mbio kwenda kwenye ng'ombe, akachukua ndama mwanana mwenye nyama nzuri, akampa kijana, naye akaenda kuitengeneza vizuri. 8Kisha Aburahamu akawaandalia siagi na maziwa na nyama za ndama, yule alizozitengeneza, nao wakala, mwenyewe akisimama karibu yao chini ya mti.
9Kisha wakamwuliza: Mkeo Sara yuko wapi? Akajibu: Yumo hemani. 10Akamwambia: Nitakaporudi kwako siku zizi hizi za mwaka ujao, ndipo, mkeo Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume. Naye Sara aliyasikia, maana alikuwa nyuma yake hapo pa kuingia hemani.#1 Mose 17:19; Rom. 9:9. 11Lakini Aburahamu na Sara walikuwa wazee wenye siku nyingi, naye Sara alikuwa amekoma kupatwa na yale mambo ya kike. 12Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake kwamba: Hivyo, nguvu za mwili wangu zilivyokwisha kupotea, nitawezaje kuipata hiyo furaha? Tena bwana wangu naye ni mzee.#1 Mose 17:17; 1 Petr. 3:6. 13Ndipo, Bwana alipomwambia Aburahamu: Mbona Sara anacheka kwamba: Kumbe mimi nitazaa kweli, nami ni mzee? 14Je? Liko jambo linalomshinda Bwana? Wakati, nitakaporudi kwako, siku zizi hizi za mwaka ujao ndipo, Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume.#Luk. 1:37. 15Lakini Sara akakana kwamba: Sikucheka, kwani aliogopa; naye akasema: Sivyo, umecheka.
Aburahamu anafumbuliwa mwangamizo wa Sodomu.
16Kisha wale waume wakaondoka huko, wakajielekeza kwenda Sodomu, naye Aburahamu akaenda nao, awasindikize. 17Bwana akasema: Nitamfichaje Aburahamu ninayotaka kuyafanya? 18Maana Aburahamu atakuwa taifa kubwa lenye nguvu, namo mwake ndimo, mataifa yote ya nchini yatakamobarikiwa.#1 Mose 12:3. 19Kwani ninamjua, ya kuwa atawaagiza wanawe nao wa mlango wake wajao nyuma yake, waishike njia ya Bwana na kufanya yaongokayo nayo ya kweli, Bwana apate kumtimizia Aburahamu aliyomwagia.#5 Mose 6:7; 32:46. 20Kwa hiyo Bwana akasema: Makelele ya Sodomu na ya Gomora ni mengi, nayo makosa yao ni mazito mno.#1 Mose 19:13. 21Nimeshuka, nitazame, kama hayo yote, ambayo niliyasikia makelele yao, wameyafanya kweli, au kama hawakuyafanya, nijue.#1 Mose 11:5; Sh. 34:16-17. 22Kisha wale watu wakageuka hapo kwenda Sodomu, lakini aburahamu akasalia hapo akisimama mbele ya Bwana.#1 Mose 19:1.
Aburahamu anawaombea Wasodomu
23Aburahamu akafika karibu, akauliza: Utamwondoa mwongofu pamoja naye asiyekucha?#4 Mose 16:22; 2 Sam. 24:17. 24Labda mle mjini wamo waongofu 50; basi, utawaondoa nao? Hutapahurumia mahali hapo kwa ajili ya waongofu 50 waliopo? 25Jambo kama hilo halipasi kabisa, ulifanye, ukimwua mwongofu pamoja naye asiyekucha, mwongofu akiwa kwako kama mwingine asiyekucha. Hili halikupasi kabisa wewe utakayewaamua walimwengu wote, hayo si maamuzi, utakayoyaamua. 26Bwana akasema: Kama nitawaona waongofu 50 mle mjini mwa Sodomu, nitapahurumia mahali pale pote kwa ajili yao.#Yes. 65:8; Ez. 22:30; Mat. 24:22. 27Aburahamu akajibu kwamba: Tazama nimejipa moyo wa kusema na Bwana, ingawa mimi ni mavumbi na majivu. 28Labda wale waongofu 50 wamepunguka watano, sasa utaungamiza mji wote kwa ajili ya hao watano? Akasema: Sitauangamiza, kama nitaona humo 45. 29Akaendelea kusema naye kwamba: Labda wataonekana humo 40 tu. Akasema: Sitafanya kitu kwa ajili yao hao 40. 30Akasema: Makali ya Bwana yasiwake moto, nikisema tena: Labda wataonekana humo 30 tu. Akasema: Sitafanya kitu, kama nitaona humo 30 tu.#Amu. 6:39. 31Akasema: Tazama, nimejipa moyo wa kusema na Bwana: Labda wataonekana humo 20 tu. Akasema: Sitauangamiza kwa ajili yao hao 20. 32Akasema: Makali ya Bwana yasiwake moto, nikisema tena mara moja tu: Labda wataonekana humo 10 tu. Akasema: Sitauangamiza kwa ajili yao hao 10 tu. 33Bwana alipokwisha kusema na Aburahamu akaenda zake, naye Aburahamu akarudi mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 18: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia