1 Mose 13
13
Aburamu na Loti wanatengana.
1Ndipo, Aburamu alipotoka Misri kwenda kwao upande wa kusini, yeye na mkewe nao wote, aliokuwa nao, hata Loti alikuwa naye. 2Naye Aburamu alikuwa mwenye mali nyingi sana za makundi na za fedha na za dhahabu.#Fano. 10:22. 3Akaendelea kusafiri hapohapo upande wa kusini mpaka kufika Beteli mahali pale, hema lake lilipokuwa kwanza katikati ya Beteli na Ai; 4ndipo hapo, Aburamu alipojenga pa kwanza pa kumtambikia Bwana na kulitambikia Jina lake.#1 Mose 12:8. 5Lakini Loti naye aliyesafiri pamoja na Aburamu alikuwa mwenye mbuzi na kondoo na ng'ombe na mahema. 6Kwa hiyo haikuwezekana, wakae pamoja katika nchi ile, kwa kuwa mapato yao yalikuwa mengi, kweli hawakuweza kukaa pamoja. 7Kwa hiyo wachunga makundi ya Aburamu waligombana nao wachunga makundi ya Loti, kwani Wakanaani na Waperizi nao walikaa siku zile katika nchi hiyo. 8Ndipo, Aburamu alipomwambia Loti: Tusigombane mimi na wewe, wala wachungaji wangu na wachungaji wako! Kwani sisi tu ndugu.#Sh. 133:1. 9Huoni nchi yote iliyoko mbele yako? Na tutengane! Ukitaka kushotoni, nitakwenda kuumeni; ukitaka kuumeni, nitakwenda kushotoni. 10Loti akayainua macho yake, akaliona bonde zima la Yordani, ya kuwa lote lilikuwa lenye maji mengi kufika hata Soari; Bwana alipokuwa hajaiangamiza bado Sodomu na Gomora, lilikuwa kama shamba la Mungu, kama Misri. 11Kwa hiyo Loti akajichagulia hilo bonde zima la Yordani, kisha Loti akaondoka kwenda huo upande wa maawioni kwa jua. Hivyo ndivyo, hao ndugu walivyotengana. 12Aburamu akakaa katika nchi ya Kanaani, naye Loti akakaa katika miji ya hilo bonde, akaenda kuyapiga mahema yake mpaka Sodomu. 13Lakini watu wa Sodomu walikuwa wabaya, wakamkosea Bwana sana.#1 Mose 18:20; 19:4-9.
Kiagio cha pili, Mungu alichompa Aburamu.
14Aburamu alipokwisha kutengana na Loti, Bwana akamwambia: Yainue macho yako, utazame toka mahali hapa, unapokaa, upande wa kaskazini na wa kusini na wa maawioni kwa jua na wa baharini! 15Nchi hizi zote, unazoziona, nitakupa wewe nao wa uzao wako kuwa zenu kale na kale.#1 Mose 12:7. 16Nao wazao wako nitawafanya kuwa wengi kama mavumbi ya nchi. Kama mtu anaweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, wa uzao wako nao watahesabika.#1 Mose 28:14; 4 Mose 23:10. 17Inuka, utembee katika nchi hii kuuona urefu wake na upana wake! Kwani ndiyo, nitakayokupa wewe. 18Kisha Aburamu akayafunga mahema, akaenda kukaa katika kimwitu cha Mamure kilichokuwa karibu ya Heburoni, akajenga huko pa kumtambikia Bwana.#1 Mose 14:13,24.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 13: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.