Matendo ya Mitume 11
11
Petero anayaeleza mambo ya Kornelio.
1Mitume na ndugu waliokuwako Yudea wakasikia, ya kuwa hata wamizimu wamelipokea Neno la Mungu.#Tume. 10:45. 2Petero alipopanda kwenda Yerusalemu, waliotahiriwa wakabishana naye wakisema: 3Umeingia mwa watu wasiotahiriwa, ukala pamoja nao.#Gal. 2:12. 4Petero akaanza kuwaeleza yote, yalivyofuatana, akisema: 5Mimi nilipokuwa katika mji wa Yope nikimwomba Mungu, nikaingiwa na kituko kwa kuona njozi: chombo kinachofanana na guo kubwa linatelemshwa chini toka mbinguni likishikwa kwa pembe zake nne likaja mpaka hapo, nilipokuwa.#Tume. 10:9-48. 6Nami nilipochungulia mle nikitazama, nikaona, mna nyama wenye miguu minne wa nchini nao nyama wa mwituni nao watambao nao ndege wa angani; 7kisha nikasikia sauti ya kuniambia: Inuka, Petero, uchinje, ule! 8Ndipo, niliposema: Hapana, Bwana, kwani cho chote kilicho chenye mwiko au kisichotakata hakijaingia bado kinywani mwangu. 9Lakini sauti ikanijibu tena toka mbinguni: Mungu alivyovitakasa, wewe usivizie! 10Vikafanyika hivyo mara tatu, kisha yote yakavutwa tena na kupazwa mbinguni. 11Mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba, nilimokuwa, walitumwa kwangu toka Kesaria. 12Naye Roho akaniambia, niende pamoja nao pasipo mashaka; hata hawa ndugu sita wakafuatana nami, tukaingia nyumbani mwake yule mtu. 13Huyo akatusimulia, alivyoona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kusema: Tume watu, waende Yope, wamwite Simoni anayeitwa Petero! 14Ndiye atakayekuambia maneno yatakayokuokoa wewe nao wote wa nyumbani mwako. 15Nami nilipoanza kusema, Roho Mtakatifu akawaguia, kama alivyotuguia hata sisi hapo kwanza.#Tume. 2:1-4. 16Ndipo, nilipolikumbuka neno la Bwana, alilolisema: Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatiza katika Roho takatifu.#Tume. 1:5. 17Mungu alipowapa kipaji kilekile, tulichokipata na sisi tuliomtegemea Bwana Yesu Kristo, hapo mimi nilikuwa na nguvu gani, niweza kumzuia Mungu? 18Walipoyasikia haya wakanyamaza kimya, wakamtukuza Mungu wakisema: Kumbe hata wamizimu Mungu amewapa majuto, nao wapate uzima!
Wateule wa Antiokia.
19Wale waliotawanyika kwa sababu ya maumivu, waliyopatwa nayo, Stefano alipouawa, wakazunguka, wakafika mpaka Ufoniki na Kipuro na Antiokia, wasimwambie mtu hilo Neno pasipo Wayuda peke yao.#Tume. 8:1-4. 20Lakini wengine wao walikuwa watu wa Kipuro nao wa Kirene. Hao walipofika Antiokia, wakawapigia hata Wagriki mbiu njema ya Bwana Yesu. 21Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, wakawa wengi waliomgeukia Bwana kwa kumtegemea.#Tume. 2:47. 22Hilo neno lao liliposikilika masikioni pa wateule waliokuwa huko Yerusalemu, wakamtuma Barnaba, aende Antiokia.#Tume. 4:36. 23Naye alipofika na kuviona vipaji, Mungu alivyowagawia, akafurahi, akawahimiza wote, wakaze mioyo kushikamana na Bwana.#Tume. 13:43. 24Kwa kuwa mtu mwema aliyejaa Roho takatifu alizidi kumtegemea Mungu; kwa hiyo kikundi kizima cha watu kikapelekwa kwa Bwana.#Tume. 6:5; 5:14. 25Kisha akatoka kwenda Tarso kumtafuta Sauli;#Tume. 9:30. 26alipomwona akampeleka Antiokia. Kisha wakakaa nao wateule wa hapo hata mwaka mzima, wakafundisha watu wengi; napo hapo Antiokia ndipo, wanafunzi walipoanza kuitwa Wakristo.#Gal. 2:11.
27Ikawa siku zile, wakashuka wafumbuaji toka Yerusalemu kufika Antiokia.#Tume. 13:1; 15:32. 28Mmoja wao, jina lake Agabo, akainuka kwa kuongozwa na Roho, akaonyesha, kwamba itakuwa njaa kubwa ulimwenguni mote; nayo ikawako siku za Klaudio.#Tume. 21:10. 29Ndipo, wanafunzi walipopatana, kwamba kila mtu kwa hivyo, alivyofanikiwa, atoe mali, zipelekwe za kuwatumikia ndugu waliokaa Yudea.#Gal. 2:10. 30Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.#Tume. 12:25; 1 Kor. 16:1; Gal. 2:10.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo ya Mitume 11: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.