Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko MT. 2

2
1AKAINGIA Kapernaum tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. 2Marra wakakusanyika watu wengi isibaki nafasi hatta mlangoni: akasema nao neno lake. 3Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wane. 4Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu va makutano, wakaitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakakitelemsha kitanda alichokilalia yule mwenye kupooza. 5Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, dhambi zako zimeondolewa. 6Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, 7Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezae kuondoa dhambi isipokuwa mmoja, ndive Mungu? 8Marra Yesu akafahamu rohoni mwake kama wanafikiri hivi nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? 9Vipi vyepesi, kumwambia mwenye kupooza, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, njitwike kitanda chako, ukaenende? 10Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dbambi (amwambia yule inwenye kupooza), 11Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako. 12Akaondoka marra, akajitwika kitanda chake, akatoka mbele yao wote; hatta wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakinena, Namna hii hatujapata kuyaona kamwe.
13Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, makutano yote wakamwendea, akawafundisha. 14Hatta alipokuwa akipita akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata. 15Hatta alipokuwa akila nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake: kwa maana walikuwa wengi wakamfuata. 16Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 17Yesu aliposikia akawaambia, Wenye afya hawabitaji tabibu bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dbambi wapate kutubu.
18Wanafunzi wake Yohana nao wa Mafarisayo walikuwa wakifunga: wakaja, wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wra Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? 19Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kufunga maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Maadam Bwana arusi yupo pamoja nao hawawezi kufunga. 20Lakini siku zitakuja atakapoondolewa Bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile. 21Hakuna mtu ashonae kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu: ikiwa ashona, kile kipya kilicholiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipolatuka huzidi. 22Wala hapana mtu atiae divai mpya katika viriba vikuukuu: ikiwa atia, ile divai nipya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya.
23Hatta alipokuwa akipita katika makonde siku ya sabato, wanafunzi wake wakaanza kuendelea wakivunja masuke. 24Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanatenda lisilo halali siku ya sabato? 25Akawaambia, Hamkusoma kabisa alivyofanya Daud, alipokuwa ana haja, akaona njaa, yeye na wenziwe? 26Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiatbar, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa illa na makuhani, akawapa na wenziwe? 27Akawaambia, Sabato ilikuwa kwa ajili ya mwana Adamu, si mwana Adamu kwa ajili ya sabato. 28Bassi yeye aliye Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.

Iliyochaguliwa sasa

Marko MT. 2: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia