Marko MT. 10
10
1AKAONDOKA huko akafika mipaka ya Yahudi kwa niia ya ngʼambu ya Yardani; watu wengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea. 2Mafa risayo wakamwendea, wakamwuliza, Ni balali mtu kumwaeha mkewe? wakimjaribu. 3Nae akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini? 4Wakasema, Musa alitoa rukhusa kuandika khati ya talaka na kumwacha. 5Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yemi aliwaandikia amri hii. 6Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, Mungu aliwafanya mtu mume na mtu mke. 7Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe: 8na hawo wawili watakuwa mwili mmoja; hatta wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9Bassi alivyoviunganisha Mungu, mwana Adamu asivitenganishe. 10Hatta nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza khabari ya neno hilohilo. 11Akawaambia, Killa mtu atakaemwacha mkewe na kuoa mwingine azini na kumkosa: 12na mke, akimwacha mume wake na kuolewa na mtu mwingine, azini.
13Wakamletea watoto wachanga illi awaguse: wanafunzi wake wakawakemea wao waliowaleta. 14Lakini Yesu alipoona akachukiwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wachanga waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawo ufalme wa mbinguni ni wao. 15Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali nfalme wa Mungu kama mtoto mchanga hatauingia kabisa. 16Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
17Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele? 18Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. 19Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Usidanganye, Waheshimu haha yako na mama yako. 20Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu ujana wangu. 21Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate. 22Walakini yeye akakunja uso kwa neno lile, akaenda zake kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
23Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Kwa shidda gani wenye mali wataingia katika ufalme wa Mungu! 24Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, kwa shidda gani wenye kuitegemea mali wataingia katika ufalme wa Mungu! 25Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 26Nao wakashangaa mno, wakiambiana, Nani, bassi, awezae kuokoka? 27Yesu akawakazia macho, akanena, Kwa wana Adamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. 28Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. 29Yesu akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, Hapana mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume au ndugu wake, au baba, au mama, au mke, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, au kwa ajili ya Injili, 30illa atapewa marra mia sasa wakati huu, nyumba na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na mateso: na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. 31Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho: na wa mwisho wa kwanza.
32Wakawa njiani, wakipanda kwenda Yerusalemi; na Yesu alikuwa akiwatangulia: wakashangaa, na wakifuata wakaogopa. Akawachukua tena wale thenashara akaanza kuwaambia khabari za mambo yatakayompata, akinena, 33Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi: na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi, 34na watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa mataifa, nao watamdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumtemea mate, na kumwua: na siku ya tatu atafufuka.
35Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakimwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba. 36Akawaambia, Mwalaka niwafanyie nini? 37Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto katika utukufu wako. 38Yesu akawaambia, Hamjui mnaioliomba. Mnaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, na kubatizwa nbatizo nibatizwao mimi? 39Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa: 40bali khabari ya kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapeni, illa wao watapewa waliowekewa tayari. 41Hatta wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 42Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa majumbe wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 43Lakini haitakuwa hivi kwemi; bali mtu atakae kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mkhudumu wenu, 44na mtu atakae kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. 45Kwa maana Mwana wa Adamu nae hakuja kukhudumiwa bali kukhudumu, na kutoa roho yake iwe dia ya wengi.
46Wakafika Yeriko: hatta alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka. 47Aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, akaanza kupaaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daud, Yesu, unirehemu. 48Yesu akasimama akaagiza aitwe. 49Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; ondoka, anakuita. 50Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. 51Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyieni? Yule kipofu akamwambia, Rabbi, nipate kuona tena. 52Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Marra akapata kuona tena; akafuata Yesu njiani.
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 10: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.