Mattayo MT. 19
19
1IKAWA Yesu alipomaliza maneno haya, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Yahudi, ngʼambu ya Yordani. 2Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.
3Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je, ni halali mtu kumwacha mkewe kwa killa sababu? 4Akajihu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5akasema. Kwa sababu hii, mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe; na hawo wawili watakuwa mwili mmoja? 6Hatta wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Bassi alivyoviunganisha, Mungu, mwana Adamu asivitenganishe. 7Wakamwambia, Jinsi gani bassi Musa aliamuru kumpa khati ya talaka, na kumwacha? 8Akawaambia, Musa kwa sabau ya ugumu wa mioyo yenu aliwapeni ruksa kuwaacha wake zenu: lakini langu mwanzo haikuwa hivi. 9Nami nawaambia ninyi, Killa mtu atakaemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya asharati, akaoa mwingine, azini; nae amwoae yule aliyeachwa azini. 10Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa liivi, haifai kuoa. 11Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, illa wale waliojaliwa. 12Maana wako matawashi waliozaliwa katika hali hii toka matumboni mwa mama zao; teua wako matawashi waliofanywa kuwa matawashi na watu: tena wako matawashi waliojifanya kuwa matawashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezae kulipokea neno hili, na alipokee.
13Ndipo akaletewa vitoto aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea. 14Lakini Yesu akasema, Waacheni vitoto, wala msiwakataze kuja kwangu; kwa maana walio mfano wa hawo, ufalme wa mbinguni ni wao. 15Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.
16Mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu mwema, nitende jambo gani jema, illi nipate uzima wa milele? 17Akamwambia, Ya nini kuniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. Lakini ukitaka kuingia katika nzima, zishike amri. 18Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo, 19Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 20Yule kijima akamwambia, Haya yote nimeyashika tangu utoto wangu: nimepmigukiwa nini tena? 21Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate. 22Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali mengi.
23Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shidda tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24Nawaambieni tena, Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 25Wanafunzi wake waliposikia, wakashangaa sana, wakinena, Nani bassi awezae kuokoka? 26Yesu akawatazama, akawaambia, Kwa wana Adamu hili haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
27Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata: tutapata nini bassi? 28Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli. 29Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele. 30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho, wa kwanza.
Iliyochaguliwa sasa
Mattayo MT. 19: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.