Mattayo MT. 16
16
1WAKAMJIA Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. 2Akajibu, akawaambia, Kukichwa, mwanena, Kutakuwa na kianga: kwa maana uwingu ni mwekundu. 3Na assubuhi, Leo dhoruba; kwa maana uwingu ni mwekundu, na kumetanda. Enyi wanafiki, mnajua kuutamhua uso wa uwingu; hali ishara za zamani hizi hamziwezi. 4Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake.
5Wanafunzi wake wakaenda hatta ngʼambu, wakasahau kuchukua mikate. 6Yesu akawaambia, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masudukayo. 7Wakabishana wao kwa wao, wakinena, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. 8Yesu akajua, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamkuchukua mikate? 9Hamjafahamu hado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyookota? 10Wala ile mikate saba kwa wale elfu nne, na makanda mangapi mliyookota? 11Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo? 12Ndipo wakafahamu ya kuwa hakuwaambia kujihadhari na chachu ya mkate, bali elimu ya Mafarisayo na Masadukayo.
13Yesu akaenda pande za Kaisaria Filipi, akawauliza wanafunzi wake akinena, Watu huninena mimi, Mwana wa Adamu, kuwa nani? 14Wakasema, Wengine Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15Akawaambia, Na ninyi mwaninena mimi kuwa nani? 16Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi. 17Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda. 19Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litafungwa mbinguni: na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20Ndipo akawaagiza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ya kwamba yeye ndiye Yesu aliye Kristo.
21Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 22Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akinena, Hasha, Bwana, haya hayatakupata. 23Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu. 24Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25Maana mtu atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza; na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu, ataiona. 26Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake? 27Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake. 28Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
Iliyochaguliwa sasa
Mattayo MT. 16: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.