Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mattayo MT. 14

14
1WAKATI ule Herode tetrarka alisikia khabari za Yesu, 2akawaambia watumishi wake, Huyu ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa sababu hii nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. 3Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo ndugu yake. 4Kwa sababu Yohana alimwambia, Ni haramu kwako kukaa uae. 5Na alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona kuwa nabii. 6Hatta panapo siku kuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodias alicheza kati ya watu, akampendeza Herode. 7Hatta akakiri kwa kiapo atampa lo lote atakaloliomba. 8Nae, akishawishwa na mama yake, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. 9Mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya nyapo zake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja nae, akaamuru apewe; 10akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. 11Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana: akakichukua kwa mama yake. 12Wanafunzi wake wakaenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika; wakaenda wakampasha Yesu khabari.
13Yesu aliposikia, akatoka huku katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, kwa faragha. Na makutano waliposikia, wakamfuata kwa miguu toka miji yao. 14Yesu akatoka, akaona makutano mengi, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. 15Hatta ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamwendea, wakanena, Mahali hapa nyika tupu, na saa imekwisha pita; waage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. 16Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi kula. 17Wakamwambia, Hatuna kitu hapa illa mikate mitano na samaki mbili. 18Akasema, Nileteeni vitu vile hapa. 19Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akamega, akawapa wanafunzi ile mikate, wanafunzi wakawapa makutano. 20Wakala wote wakashiba: wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu thenashara, vimejaa. 21Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
22Marra Yesu akawalazimisha wamifunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ngʼambu, wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano. 23Alipokwisha kuwaaga makutano, akapanda mlimani kwa faragha, kwenda kusali.
Na ilipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. 24Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho. 25Hatta zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akitembea juu ya bahari. 26Wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, wakafadhaika, wakinena. Ni kivuli; wakapiga yowe kwa khofu. 27Marra Yesu akasema nao, akinena, Jipeni moyo; ni mimi; msiogope. 28Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akatembea juu ya maji, illi kumwendea Yesu. 30Lakini alipoona upepo wa nguvu, akaogopa: akaanza kuzama, akapiga yowe, akinena, Bwana, niokoe. 31Marra Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? 32Walipopanda chomboni, upepo ukakoma. 33Nao waliokuwa ndani ya chombo wakamwendea, wakamsujudia, wakinena, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.
34Na walipokwisha kuvuka, wakafika inchi ya Genesareti. 35Na watu wa mahali pale walipomtambua, wakatuma watu kwenda inchi zile zote zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; 36wakamsihi waguse hatta pindo la vazi lake; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.

Iliyochaguliwa sasa

Mattayo MT. 14: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia