Yohana 14
14
Yesu ni njia ya kwenda kwa Baba
1 #
Yn 14:27; Mk 11:22 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3#Yn 12:26; 17:24 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. 4Nami niendako mwaijua njia. 5Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia? 6#Ebr 10:20; Mt 11:27; Yn 11:25; Rum 5:1,2 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 8Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. 9#Yn 12:45; Ebr 1:3; Mt 17:17 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? 10#Yn 12:49 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 11#Yn 14:20; 10:25,38 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12#Mk 16:19,20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13#Yn 15:7; Mk 11:24; 1 Yoh 5:14 Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14#Yn 16:23,24 Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.
Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu
15 #
Yn 15:10; 1 Yoh 5:3 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16#Yn 14:26; 15:26; 16:7; 1 Yoh 2:1 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17#Yn 7:39; 16:13; Mt 10:20; Rum 8:26 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 19#Yn 16:16 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20#Yn 17:21-23 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21#2 Kor 3:18; 1 Yoh 5:3 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 22#Mdo 10:41 Yuda (siye Iskarioti), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23#Yn 13:34; 14:21; Mit 8:17; Mt 18:20; 28:20; Efe 3:17; 2 Kor 6:16 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24#Yn 7:16; 1 Yoh 2:5 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenituma.
25Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26#Yn 14:16; Mt 10:19 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27#Yn 1:16,33; Flp 4:7 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28#Yn 14:3,6,18; Lk 24:52 Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29#Yn 13:19 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, ili litakapotokea mpate kuamini. 30#Yn 12:31; Efe 2:2 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31#Yn 10:18; Mt 26:46; Mk 14:42 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 14: RSUVDC
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.