Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 6

6
Suala juu ya siku ya Sabato#6:1 Siku moja ya Sabato: Hati nyingine za mkono hapa zina maneno ambayo si dhahiri kueleweka pengine: Sabato ya pili baada ya kwanza au: Sabato iliyokuwa baada ya iliyofuata.
(Mat 12:1-8; Marko 2:23-28)
1Siku moja ya Sabato,#6:1-5 Sehemu hii na ifuatayo (aya 6-11) zinasema juu ya ubishi kati ya Yesu na Mafarisayo kuhusu kuzingatia miiko ya Sabato. Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala. 2Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato?” 3Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? 4Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu,#6:4 Mikate iliyowekwa mbele ya Mungu: Kila siku ya sabato mikate mipya kumi na miwili iliwekwa juu ya meza ya dhahabu hekaluni, na ile iliyokuwapo juma lililopita makuhani waliweza kuila (Lawi 24:5-9). akala na kuwapa wenzake. Haikuruhusiwa mtu kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani.” 5Hivyo akawaambia, “Mwana wa Mtu ana uwezo juu ya Sabato.”#6:5 Hati moja ya kale inaiweka aya hii baada ya aya ya 10 na mahala pake hapa imeingiza kisa hiki: Na siku moja Yesu alipomwona mtu mmoja anafanya kazi siku hiyo ya Sabato akamwambia: “Ewe mtu! Kama unajua unachofanya basi una heri; la hujui, basi umelaaniwa kwani ni mvunja sheria.”
Mtu mwenye mkono uliopooza
(Mat 12:9-14; Marko 3:1-6)
6Siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia katika sunagogi, akafundisha. Mle ndani kulikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza. 7Waalimu wa sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisa cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.#6:7 Mafarisayo walifikiri imekatazwa kumponya mtu siku ya Sabato. 8Lakini Yesu alijua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Inuka, simama katikati.” Yule mtu akaenda kusimama katikati. 9Kisha Yesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?” 10Baada ya kuwatazama wote waliokuwa pale, akamwambia yule mtu,#6:10 Akamwambia yule mtu …: Hati nyingine za mkono zina: akamwambia yule mtu kwa ukali. “Nyosha mkono wako.” Naye akafanya hivyo, na mkono wake ukawa mzima tena. 11Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu.
Yesu anateua mitume kumi na wawili
(Mat 10:1-4; Marko 3:13-19)
12Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akisali.#6:12 Akakesha huko usiku kucha akisali: Angalia maelezo ya 3:21. Taz pia Mat 14:23 na Luka 9:28. 13Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume:#6:13 Katika kundi la watu wengi ambao walimfuata Yesu, Yesu aliwachagua watu 12 ambao aliwapa jina mitume, neno ambalo lina maana ya waliotumwa au wajumbe. Idadi hiyo ya watu kumi na wawili inatufahamisha uundaji wa jumuiya mpya ya watu wa Mungu — namba 12 itatumiwa kuhusu makabila 12 ya Waisraeli (22:30). 14Simoni (ambaye Yesu alimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo,#6:14 Kibiblia, kumpa mtu jina ni kuonesha pia kwamba mpaji anayo mamlaka juu ya mpewa jina. Jina lingine lagusia hali mpya au malengo mapya ya huyo anayepewa jina hilo. 15Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo#6:15 Yuda mwanaye Alfayo: Au: Yuda nduguye Alfayo. na Simoni (aliyeitwa Zelote),#6:15 Zelote: Kigiriki cha neno “Mkanaani” (taz Marko 3:18); yote mawili yana maana ya “mwanamapinduzi mwenye bidii”. Jina hilo walipewa pia watu wa kikundi cha Kiyahudi ambacho kiliuasi utawala wa Waroma. 16Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti.
Yesu anafundisha na kuwaponya watu
(Mat 4:23-25)
17Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.#6:17-49 Ling aya 17-49 na mafundisho ya Yesu katika Mat 5—7. 18Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu. 19Watu wote walitaka kumgusa, kwa maana nguvu ilikuwa inatoka ndani yake na kuwaponya wote.
Heri na ole
(Mat 5:1-12)
20 # 6:20 Kama pengine pengi wanafunzi si tu wale kumi na wawili bali pia wafuasi wake Yesu kwa jumla. Yesu akawageukia wanafunzi wake, akasema:
“Heri#6:20-26 Heri: Muundo wa kimaandishi ambao hapa twaweza kuupa jina “Heri” unapatikana mahala pengine kadhaa katika Zaburi na vitabu vingine vya A.K. (Zab 1:1; 32:1-2; Meth 8:32,34; Isa 56:2). Baadhi ya heri hizi (na hasa katika Mat 5:3-12) zinasema mambo ambayo mara nyingi ni magumu kuyaelewa lakini yote yanaelezea ukweli wa ufalme wa Mungu. Kwa hizo “heri” nne zinazotajwa hapa, Luka pia anaweka “ole” nne za aya 24-26. nyinyi mlio maskini,
maana ufalme wa Mungu ni wenu.#6:20-28 Sehemu hii, zaidi kuliko sehemu sambamba katika Mat 5:3-10, inakazia msimamo wa Yesu wa kuwajali sana maskini kwa kutaja katika aya 20-21a juu ya umaskini kwa maana ya kutokuwa na kitu.
21Heri nyinyi mnaosikia njaa sasa,
maana baadaye mtashiba.
Heri nyinyi mnaolia sasa,
maana baadaye mtacheka kwa furaha.
22“Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu. 23Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
24Lakini ole wenu nyinyi mlio matajiri,
maana mmekwisha pata faraja yenu.
25Ole wenu nyinyi mnaoshiba sasa,
maana baadaye mtasikia njaa.
Ole wenu nyinyi mnaocheka kwa furaha sasa,
maana baadaye mtaomboleza na kulia.
26Ole wenu nyinyi iwapo watu wote wanawasifu,
maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.
Kuwapenda maadui
(Mat 5:38-48; 7:12a)
27“Lakini nawaambieni nyinyi mnaonisikiliza, wapendeni maadui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni. 28Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. 29Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie pia la pili. Mtu akikunyang'anya koti lako mwachie pia shati#6:29 Koti …pia shati: Koti lilivaliwa juu ya nguo nyingine; kwa hiyo hapa maana ni kwamba amwachie achukue na hiyo nguo ya ndani iliyobakia. lako. 30Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang'anya mali yako usimtake akurudishie. 31Jinsi mnavyotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo.#6:31 Mwongozo huu mzuri ulijulikana miongoni mwa Wayahudi na watu wengine hata wa kwetu. Kawaida ulikuwa unatajwa kwa maneno: Msi …, lakini Yesu hapa anasema: Watendeeni … Yaani anasisitiza kutenda na siyo kuacha kutenda.
32“Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao. 33Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo. 34Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile. 35Ila nyinyi wapendeni maadui zenu na kuwatendea mema; kopesheni bila kutazamia kurudishiwa, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya. 36Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.
Juu ya kuwahukumu wengine
(Mat 7:1-5)
37“Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa.#6:37 Nanyi hamtahukumiwa: Yaani na Mungu ambaye ndiye mwenye kuhukumu. Matumizi ya hali ya kutendewa mara nyingi mwenye kutenda ndiye Mungu. Kwa hiyo tafsiri: Nanyi hamtahukumiwa na Mungu ni sawa. 38Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu#6:38 Mifukoni mwenu: Neno kwa neno: Kifuani mwenu, kwa vile kulingana na desturi, watu wakiokota nafaka waliiweka katika mifuko waliyoifanya kwa kupindia kifuani shuka walizovaa au mavazi waliyovaa. kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho atakachotumia Mungu kwenu.”
39Akawaambia mfano huu: “Je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake? La! Wote wataanguka shimoni. 40Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akisha hitimu huwa kama mwalimu wake. 41Kwa nini wakiona kibanzi jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? 42Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.
Mtu hujulikana kwa matunda yake
(Mat 7:16-20; 12:33-35)
43“Mti mzuri hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri. 44Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili. 45Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
Wajenzi wa namna mbili
(Mat 7:24-27)
46“Mbona mwaniita ‘Bwana, Bwana,’ na huku hamtimizi yale ninayosema? 47Nitawapeni mfano unaofaa kuonesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza: 48Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara. 49Lakini yeyote anayesikia maneno yangu asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”

Iliyochaguliwa sasa

Luka 6: BHNTLK

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia