Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohane 10

10
Mchungaji mwema#10:1-21 Mchungaji Mwema: Katika Injili tatu za Sunoptiki Yesu anafundisha mara nyingi kwa kutumia mifano. Hapa tunapewa mfano mmoja tu katika Injili hii ya Yohane. Katika A.K. Mungu anatajwa mara kwa mara kama mchungaji na watu kama kondoo wa Mungu (Zab 23:1; 77:20; 79:13; 95:7; 100:3; Isa 40:11; Yer 23:1-6; Eze 34:11-31; 37:24). Katika A.J. picha hiyo inatumiwa kwa Yesu Kristo (Mat 9:36; 18:12-14; Marko 6:34; Luka 15:4-7; Ebr 13:20; 1Pet 2:25; 5:4; Ufu 7:17) na pia kwa wachungaji wa kanisa (taz Yoh 21:15 maelezo). Katika mfano huu maarufu Yesu anatumia vielelezo vya mchungaji, kundi na wezi kuelezea uhusiano uliopo kati yake, wafuasi wake wa kweli, na wote ambao watahusika katika uhusiano wa Mungu na watu wake.
1“Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi. 2Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo. 3Mngojamlango#10:3 Mngojamlango: Huyo mngojamlango anaweza pia kuwa ndiye mchungaji mwenyewe. Ana uwezo wa kuthibiti ni nani anayeingia na kutoka katika zizi la kondoo. Anawahesabu pia kondoo waliomo, wanapotoka na wanapoingia. Mlango ndiyo njia ya pekee ya kuingia na kutoka zizini. wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake;#10:3 Kondoo husikia sauti yake: Katika Biblia kondoo na kundi la kondoo hutumika kama mfano wa watu wa Mungu. Na picha au mfano wa “Mchungaji Mwema” ulitumika tangu mwanzoni mwa Kanisa kumtaja Yesu Kristo. naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake, na kuwaongoza nje. 4Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake. 5Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.” 6Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
Yesu mchungaji mwema
7Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.#10:7 Mimi ni mlango wa kondoo: Tazama 6:35. Kama mlango wa kondoo, yaani wafuasi wake, Yesu ndiye njia ambayo wote wanaomwamini wanapata uwezo wa kumwendea Mungu na kuwa watu wake Mungu. Yeye huwatunza na kuwalinda. Tena ni yeye peke yake anayeamua ni nani na nani atakayepitia mlango huo. 8Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi,#10:8 Wezi na wanyang'anyi: Hapa Yesu anaongea juu ya wale ambao wamekuwa wakifundisha watu wa Mungu ile sheria ya Mose kwa namna ambayo iliwapotosha kutoka ukweli kuhusu matakwa ya Mungu. nao kondoo hawakuwasikiliza. 9Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho. 10Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uhai — uhai kamili.
11“Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo#10:11 Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo: Taz 10:15; 13:37; 15:13. wake. 12Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya. 13Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. 14Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi, 15kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao. 16Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.#10:16 Kutakuwako kundi moja na mchungaji moja: Yesu atawasaidia wafuasi wake (kondoo wake) kuwa kitu kimoja licha ya tofauti zao (taz pia Gal 3:26-29).
17“Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena. 18Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
19Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. 20Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?” 21Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”
Yesu anakataliwa na Wayahudi
22Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya kutabaruku.#10:22 Sikukuu ya kutabaruku: Sikukuu ya kukumbuka kuweka wakfu hekalu la Yerusalemu (mwaka 168 K.K.). Iliadhimishwa kwa siku 8 katika mwezi wa Desemba. Wakati huo ulikuwa wa baridi. 23Naye Yesu akawa anatembea hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.#10:23 Ukumbi wa Solomoni: Ni mahali pakubwa palipotengenezwa kwa mawe makubwa upande wa mashariki mwa hekalu katika sehemu ya ndani ya ukuta uliouzunnguka (Mate 3:11; 5:12). 24Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, basi, tuambie wazi.” 25Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia. 26Lakini nyinyi hamsadiki kwa sababu nyinyi si kondoo wangu. 27Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata. 28Mimi nawapa uhai wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu. 29Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote,#10:29 Baba yangu …aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote: Tafsiri kulingana na hati moja ya kale. Tafsiri nyingine yamkini ni: “Alichonipa Baba ni kikuu kuliko yote” na hii ina maana ya uwezo wake Yesu. wala hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba. 30Mimi na Baba, tu mmoja.”#10:30 Mimi na Baba, tu mmoja: Yesu ataeleza zaidi katika aya 34-36 juu ya uhusiano wake na Mungu na kwamba hajitakii tu kuwa sawa naye bali umoja wake na Mungu wahusu kule kuwa kwake Mwana wa Mungu na kufanya yale Mungu anayotaka ayafanye (aya 36-38).
31Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie.#10:31 Wakachukua mawe ili wamtupie: Mtu yeyote aliyekataa kutii sheria ya Mose hata kuhatarisha usafi wa kidini wa taifa ilibidi auawe kwa kupigwa mawe (Lawi 24:15-16; Kumb 21:18-21). 32Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?” 33Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa ajili ya kazi njema, ila kwa sababu ya kumkufuru Mungu!#10:33 Kumkufuru Mungu!: Kufuru ni maneno au vitendo ambavyo vinamkashifu Mungu mwenyewe na ambavyo adhabu yake ilikuwa kifo (Mat 26:65; Marko 14:64; Luka 22:70-71; rejea Lawi 24:15-16). Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu.” 34Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika sheria yenu: ‘Mimi nimesema, nyinyi ni miungu?’ 35Mungu aliwaita miungu wale waliopewa ujumbe wake; nasi twajua kwamba Maandiko Matakatifu yasema ukweli daima. 36Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu na kumtuma ulimwenguni, mnamwambia: ‘Unakufuru,’ eti kwa sababu nilisema: ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ 37Kama sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini. 38Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi, mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake.” 39Wakajaribu tena kumkamata lakini akachopoka mikononi mwao.
40Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko. 41Watu wengi walimwendea wakasema, “Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa.” 42Watu wengi mahali hapo wakamwamini.

Iliyochaguliwa sasa

Yohane 10: BHNTLK

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia