Yakobo 5
5
Onyo kwa matajiri
1Na sasa sikilizeni enyi matajiri!#5:1 Matajiri: Lengo la mwandishi sio kulaani utajiri maana utajiri au mali inaweza kutumiwa kutenda mema na kuwaondoa wengine katika taabu. Onyo ni dhidi ya wale ambao wanapenda fedha kiasi cha kuacha kutenda matakwa ya Mungu. Kadiri ya 1Tim 6:10 fedha au mali ni chanzo cha uovu wote. Lieni na kuomboleza kwa sababu ya taabu zitakazowajieni. 2Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo. 3Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto.#5:3 Itakula miili yenu kama vile moto: Yahusu hukumu ya adhabu ya mwisho wakati hakuna chochote cha kidunia alicho nacho mtu kitakachomsaidia. Nyinyi mmejirundikia mali katika siku hizi za mwisho! 4Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni mwa Bwana wa majeshi.#5:4 Aya hii inadokezea Lawi 19:13. Rejea Kumb 24:14-15; Yer 22:13. 5Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. 6Mmemhukumu na kumuua mtu asiye na hatia, naye hakuwapingeni!
Subira na sala
7Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli. 8Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia.#5:8 Maneno haya yanadokezea kuja kwake Bwana Yesu kwa utukufu. Sehemu nyingI katika A.J. zinasema juu ya kurudi kwake Yesu Kristo kuwakusanya watu wake (Mat 24:30; 1Thes 4:13-17).
9Ndugu zangu, msinung'unikiane nyinyi kwa nyinyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu#5:9 Hakimu: Yamkini 201chakimu” hapa ni Yesu Kristo (aya 8; rejea Mat 25:31; Mate 10:42); au, Mungu mwenyewe (4:12; ling Rom 2:16; Ebr 12:23). yu karibu, tayari kuingia. 10Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana. 11Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.
12Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
13Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa. 14Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa,#5:14 Wazee wa kanisa: Yaani, viongozi au wenye wadhifa wa kuiongoza jumuiya ya waumini. Taz Mate 11:30 maelezo. nao watamwombea na kumpaka mafuta#5:14 Mafuta: Yaani, mafuta ya zeituni. Mafuta hayo yalitumiwa kama dawa (rejea Luka 10:34); hapa yahusu matumizi ya hayo mafuta “kwa jina la Bwana”, yakiandamana na sala ili aweze kuponywa na Bwana (rejea Marko 6:13) na kusamehewa dhambi (rejea Mat 9:1-8). kwa jina la Bwana. 15Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa. 16Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi. 17Elia alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua isinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa mazao yake.
19Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine akamrudisha, 20fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.#5:20 Dhambi nyingi zitaondolewa: Labda msemo huu unapaswa kueleweka kwa maana ya jumla bila kufikiria ni dhambi gani zinazohusika. Rejea Meth 10:12; 1Pet 4:8. Lakini wengi huelewa kwamba anayeokolewa nafsi yake na kuondolewa dhambi nyingi ni huyo mwenye kumrudisha mtu mpotovu akaachana na uovu wake (taz Eze 33:1-9).
Iliyochaguliwa sasa
Yakobo 5: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993