Waebrania 10
10
1Kwa vile sheria ni kivuli#10:1 Kivuli: Taz Ebr 8:3-5 maelezo, na pia rejea Kol 2:17. tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu! 2Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na tambiko hizo zote zingekoma. 3Lakini tambiko hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao. 4Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
5Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia Mungu:
“Hukutaka tambiko wala sadaka,
lakini umenitayarishia mwili.#10:5 Lakini umenitayarishia mwili: Au, “Umenipa mwili”: Fungu la maneno ambalo linaafikiana na hati nyingine za tafsiri ya Kigiriki ya Septuajinta (LXX) ya Zab 40:6.
6Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi.
7Hapo nikasema:
‘Niko hapa, ee Mungu, kutimiza matakwa yako
kama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha sheria.’”
8Kwanza alisema: “Hutaki wala hupendezwi na tambiko, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na sheria. 9Kisha akasema: “Niko hapa, ee Mungu, tayari kufanya matakwa yako.” Hivyo Mungu alibatilisha tambiko za zamani na mahali pake akaweka tambiko nyingine moja.#10:9 Rejea Mat 26:39,42 na sambamba zake; Yoh 4:34; 5:30; 6:39-40. 10Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza matakwa ya Mungu, sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa ile tambiko ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha.
11Kila kuhani Myahudi hutoa huduma yake ya ibada ya kila siku na kutoa tambiko zilezile mara nyingi, tambiko ambazo haziwezi kuondoa dhambi. 12Lakini Kristo alitoa tambiko moja kwa ajili ya dhambi, tambiko ifaayo milele, kisha, akaketi upande wa kulia wa Mungu,#10:12-13 Aya hizi mbili zinamtaja Kristo pamoja na nyadhifa zake mbili: wadhifa wa kuhani na wadhifa wa mfalme (tazama Ebr 1:3). Rejea Zab 110:4. 13anangoja maadui zake wafanywe kama kibao chini ya miguu yake. 14Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao.
15Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema:
16“Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana:
Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao,
na kuziandika akilini mwao.”
17Kisha akaongeza kusema:
“Sitakumbuka tena dhambi zao,
wala vitendo vyao vya uhalifu.”
18Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa tambiko za kuondoa dhambi.
Tumkaribie Mungu
19Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu#10:19 Kwa damu ya Yesu: Ebr 6:19. tunapewa moyo thabiti#10:19 Tunapewa moyo thabiti: Tafsiri nyingine yamkini: “Tuna uhuru”; yaani, tofauti na wakati ule wa mwanzoni (kabla ya Yesu) sasa hakuna kizuizi tena (Ebr 9:7-9). wa kuingia Mahali Patakatifu.#10:19-39 Sehemu hii ambayo kwa jumla ina maneno ya kuwatia moyo waumini, inachukua mawaidha kadha wa kadha kutoka katika mafundisho yaliyotangulia ili Wakristo wayatekeleze kwa vitendo katika maisha yao. 20Yeye ametufungulia njia mpya, njia ya uhai, kupitia lile pazia,#10:20 Kupitia lile pazia: Taz Ebr 6:19. Hapa, pazia linatumika kama ishara au mfano wa mwili wake Kristo mwenyewe, ambaye kwa kifo chake alitupa uwezekano wa kwenda mbele ya Mungu (aya 5; Ebr 9:14). yaani mwili wake mwenyewe.#10:20 Mwili wake mwenyewe: Yoh 14:6; rejea Rom 5:2; Efe 2:18. 21Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. 22Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu,#10:22 Imani timilifu: Wazo hili muhimu la nafasi ya imani katika kazi ya wokovu linaingizwa hapa kama utangulizi tu wa jambo ambalo litasimuliwa kinaganaga zaidi katika sura ya 11. kwa mioyo iliyotakaswa kutokana na dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.#10:22 Miili iliyosafishwa kwa maji safi: Katika maagizo ya kuwaweka wakfu makuhani jambo la kutakaswa kwa maji (kutawadha) linatajawa katika Kut 29:4 nao walawi pia walitakaswa kwa maji ya kutakaswa (Hes 8:6-7). Rejea Eze 36:25-26; na pia Efe 5:26; 1Pet 3:21. 23Tuzingatie kabisa tumaini letu tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake ni mwaminifu. 24Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema. 25Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, siku ile ya Bwana#10:25 Siku ile ya Bwana: Katika Kigiriki tuna “siku ile” lakini kwa kawaida yahusu siku ya kuja kwake Bwana au siku ya hukumu ya mwisho. inakaribia.
26Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna tambiko iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi.#10:26-27 Taz Ebr 6:4-6 maelezo; rejea Isa 26:11. 27Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga. 28Mtu yeyote asiyetii sheria ya Mose, huuawa bila huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu. 29Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa,#10:29 Damu ya agano la Mungu iliyomtakasa: Tazama Ebr 9:20; rejea 13:20. mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani? 30Maana tunamfahamu yule aliyesema, “Mimi nitalipiza kisasi, mimi nitalipiza,” na ambaye alisema pia, “Bwana atawahukumu watu wake.”#10:30 Nukuu hizi mbili zimetolewa kutoka Kumb 32:35-36; rejea Rom 12:19. 31Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!
32Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, nyinyi mlistahimili. 33Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo. 34Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele. 35Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa. 36Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili muweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi. 37Maana kama yasemavyo Maandiko:
“Bado kidogo tu,
na yule anayekuja, atakuja,
wala hatakawia.
38Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi;
walakini akirudi nyuma,
mimi sitapendezwa naye.”
39Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa.
Iliyochaguliwa sasa
Waebrania 10: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993