Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 3

3
Petro na Yohane wanamponya kiwete
1Siku moja, saa tisa alasiri,#3:1 Saa tisa alasiri: Huo ulikuwa wakati wa pili wa siku ambao watu walitoa tambiko hekaluni na wakati wa sala ya hadhara. Petro na Yohane#3:1 Yohane: Labda mwanaye Zebedayo (Mat 4:21) ambaye alikuwa mmoja wa mitume kumi na wawili. walikuwa wakienda hekaluni, wakati wa sala. 2Wakati huo watu walikuwa wanambeba mtu mmoja kiwete tangu kuzaliwa.#3:2 Mtu kiwete alikatazwa na sheria ya Kiyahudi kuingia hekaluni (taz 2Sam 5:8). Watu hao walikuwa wakimweka huyo mtu kila siku kwenye mlango wa hekalu uitwao “Mlango Mzuri,”#3:2 Mlango Mzuri: Mlango uliokuwa upande wa mashariki wa hekalu; yamkini huo ulikuwa mlango mkuu wa kuingia katika jengo hilo. ili aombe chochote kwa wale waliokuwa wakiingia hekaluni. 3Alipowaona Petro na Yohane wakiingia hekaluni, aliwaomba wampe chochote. 4Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, “Tutazame!” 5Naye akawageukia, akitazamia kupata kitu kutoka kwao. 6Kisha Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu, lakini kile nilicho nacho nitakupa. Kwa jina#3:6 Jina: Kulingana na fikra za Kiebrania jina lilitumika katika maandishi kwa maana ya nafsi ya mtu mwenye jina hilo mwenyewe; kwa kuomba jina la Yesu Kristo watu walimwomba Yesu Kristo mwenyewe, na nguvu na uwezo wake au mamlaka yake (taz maelezo ya Mate 2:38). la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!” 7Halafu, akamshika mkono wa kulia, akamwinua. Papo hapo miguu na magoti yake yakapata nguvu. 8Akaruka, akasimama na kuanza kutembea. Halafu akaingia pamoja nao hekaluni, akitembea na kurukaruka huku akimtukuza Mungu. 9Watu wote waliokuwa hapo walimwona akitembea na kumsifu Mungu. 10Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
Hotuba ya Petro#3:11-26 Taz Mate 2:14-40 maelezo.
11Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa, wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,”#3:11 Ukumbi wa Solomoni: Ukumbi (au baraza) uliokuwa na nguzo na ambao ulikuwa upande wa ndani wa ukuta wa mashariki wa sebule ya hekalu; angalia Yoh 10:23; Mate 5:12. ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane. 12Basi, Petro alipowaona watu hao akawaambia, “Wananchi wa Israeli, kwa nini mnashangazwa na jambo hili? Mbona mnatukodolea macho kana kwamba ni kwa nguvu zetu au utakatifu wetu sisi wenyewe tumemfanya mtu huyu aweze kutembea? 13Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa babu zetu amemtukuza#3:13 Amemtukuza: Yaani, kwa ufufuo na kupaa kwake mbinguni. Angalia pia Yoh 12:16. mtumishi#3:13 Mtumishi: Matumizi ya neno hili hapa yamkini yanatukumbusha Isa 52:13 (taz pia Isa 53:11; Fil 2:7-9). Baadhi ya hati za mkono zina mwanawe, Yesu (neno la Kigiriki lililotafsiriwa kwa neno mwana ambalo laweza kuwa na maana ya mtumishi pia). wake Yesu. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.#3:13-14 Taz Mat 27:15-26 na sehemu sambamba za Injili. Maneno: “Mtakatifu na mwema” yanamtaja Yesu Kristo (Marko 1:24; Mate 7:52; 22:14; 1Yoh 2:1), nayo yana msingi wake katika fikra za A.K. (2Sam 23:3-4; Isa 32:1; 53:11; Zek 9:9). 14Alikuwa mtakatifu na mwema; lakini nyinyi mlimkataa, mkataka mtu mwingine aliyekuwa muuaji afunguliwe. 15Basi, mlimuua yule ambaye ni chanzo cha uhai. Lakini Mungu alimfufua, na sisi ni mashahidi wa tukio hilo. 16Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.#3:16 Jina ni sawa na nafsi yake huyo mwenye jina hilo haliwezi kutenganishwa naye na linachukua sifa na hali yake (taz Kut 3:13 ambapo umuhimu wa kujua jina unagusiwa. Hapa yahusu imani kwa Yesu Kristo (taz maelezo ya 3:6). Kwa kuomba kwa jina la Yesu, nguvu yake Yesu inafanya kazi kwa mwombaji 3:6; 4:7,10,30; 10:43; 16:18; 19:13.
17“Sasa ndugu zangu, mnafahamu kwamba nyinyi na wakuu wenu mlitenda hayo kwa sababu ya kutokujua kwenu. 18Lakini ndivyo Mungu alivyotimiza yale aliyotangaza zamani kwa njia ya manabii wote,#3:18 Alivyotimiza …manabii wote: Taz Yoh 20:9. Wayahudi wengi hawangeweza kufikiria na kukubali wazo la Masiha ambaye angeteseka. Lakini Wakristo, kwa upande wao, walizichukua sehemu za Zaburi na vitabu vya manabii ambazo zinasema juu ya mateso ya mtu mwadilifu wakazitumia juu ya Yesu Kristo. Isa 52:13—53:12 ni sehemu maalumu ambayo ilipata nafasi ya pekee kuhusu jambo hilo; angalia pia Mate 8:32-35. kwamba ilikuwa lazima Kristo wake ateseke. 19Basi, tubuni,#3:19 Tubuni: Kama inavyosemwa katika maneno yafuatayo, yaani “mkamrudie Mungu” ni mwito muhimu katika Biblia. mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu. 20Fanyeni hivyo ili Bwana awape nyakati za kuburudika rohoni na kuwaletea yule Kristo aliyemteua ambaye ndiye Yesu. 21Ni lazima yeye abaki huko mbinguni mpaka utakapofika wakati wa kurekebishwa vitu vyote, kama Mungu alivyosema kwa njia ya manabii wake watakatifu wa tangu zamani. 22Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe. 23Yeyote yule ambaye hatamsikiliza nabii huyo atatengwa mbali na watu wa Mungu na kuangamizwa.’ 24Manabii wote, kuanzia Samueli na wale waliomfuata, walitangaza habari za mambo haya ambayo yamekuwa yakitendeka siku hizi.#3:24 Katika mahubiri ya mwanzoni kabisa, yaani miongoni mwa Wakristo wa kwanzakwanza, lilisisitizwa jambo la kuonesha Yesu alivyokuwa ni ukamilifu wa unabii wa A.K. kwa kutumia sehemu nyingi za Zaburi ambazo zilichukuliwa kuwa za unabii. Alikuwa mzawa wa Daudi 2:29-31; 13:34; Yesu alifahamika kuwa nabii, alishika nafasi ya Mose 3:22 (Mat 16:14; Yoh 1:21) aliteseka 2:23; alikuwa jiwe walilokataa waashi lakini sasa amewekwa mahali pa heshima 4:11; alifufuka 2:25-31; 13:33-37. 25Ahadi zile Mungu alizotoa kwa njia ya manabii ni kwa ajili yenu; na mnashiriki lile agano Mungu alilofanya na babu zenu, kama alivyomwambia Abrahamu:#3:25 Alivyomwambia Abrahamu: Mwa 12:3; 22:18. ‘Kwa njia ya wazawa wako, jamaa zote za dunia zitabarikiwa.’ 26Basi, Mungu alimfufua mtumishi wake#3:26 Mtumishi wake: Taz maelezo ya 3:13. kwa faida yenu kwanza, akamtuma awaleteeni baraka kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake.”

Iliyochaguliwa sasa

Matendo 3: BHNTLK

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia