Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Sefania UTANGULIZI

UTANGULIZI
Baada ya manabii Isaya na Mika ilipita miaka kama sabini bila Yuda kuwa na nabii hadi alipotokea Sefania. Katika kipindi hicho mfalme Manase alitawala kwa muda wa miaka 55. Utawala wake ulirudisha Yuda nyuma kiroho. Desturi za dini za miungu, ukatili na mauaji vilizagaa katika utawala wake (2 Fal 21:1-18; 23:26-27). Mwanawe Amoni alipotawala alifuata mwongozo mbaya wa baba yake. Aliuawa baada ya kutawala miaka miwili tu (2 Fal 21:19-26). Yosia mwanawe akawekwa katika utawala akiwa na umri wa miaka minane (2 Fal 22:1-2). Yosia akiwa bado mdogo Sefania alianza kutoa ujumbe. Mfalme Yosia alipofikisha umri wa miaka ishirini akafanya matengenezo kidini na kisiasa.
Sefania, ambaye jina lake lina maana yake “Siri ya BWANA” au “iliyofichwa na BWANA”, aliishi Yerusalemu. Alikuwa wa jamaa ya kifalme (1:1), alikemea yaliyokuwa yamekemewa na Isaya na Mika. Ujumbe wake umekuwa utangulizi mzuri wa Nahumu, Habakuki, Obadia na Ezekieli.
Ujumbe wa Sefania ni “Siku ya BWANA” ambayo itatakasa uovu wote katika mataifa yote. Uovu wa Yuda ni kuabudu miungu na kukosa uadilifu. Yuda inatolewa wito wa kutubu (2:3). Hukumu kwa mataifa ni fundisho kwa Yuda (3:1,7,11). Sefania anaahidi wokovu kwa “mabaki” ya Yuda hasa watiifu na wanyenyekevu (3:12-13). “Mabaki” yatafurahia baraka za BWANA.
Yaliyomo:
1. Siku BWANA iliyo ya hukumu, Sura 1
2. Uhakika wa hukumu, Sura 2
3. Hukumu juu ya Yerusalemu, Sura 3:1-7
4. Ahadi ya wokovu kwa watubuo, Sura 3:8-20

Iliyochaguliwa sasa

Sefania UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia