Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria UTANGULIZI

UTANGULIZI
Katika Biblia kuna watu wapatao thelathini waitwao Zekaria. Wengi wa hao ni viongozi (2 Fal 15:8-11, 14:29), makuhani (2 Nya 24:20-26) na manabii. Kati ya manabii hao, ajulikanaye sana ni Zekaria wa kitabu hiki (1—8). Maana ya jina Zekaria ni “aliyekumbukwa na BWANA”. Zekaria mwandishi wa kitabu hiki ni wa ukoo wa makuhani (Neh 12:4,16), aliishi Yerusalemu baada ya Wayahudi kutoka uhamishoni. Alianza kutoa ujumbe akiwa bado kijana (2:4) karibu miezi miwili baada ya ujumbe wa Hagai. Zekaria na Hagai walikuwa manabii wenza waliohimiza ujenzi wa hekalu la Yerusalemu (Ezra 4:1-5, 24; 5:1-2; 6:14-15 tazama pia Utangulizi wa Hagai).
Ujumbe wa Zekaria ni faraja kwa watu waliotoka utumwani Babeli. Vile vile anahimiza uamsho wa kiroho ili wajenge hekalu upya, na kutoa unabii wa matumaini juu ya maisha. Huyu Masihi wa BWANA ataingia Yerusalemu (9:9); atauzwa kwa fedha (11:12-13, 12:10), atakufa kama mchungaji baada ya kupigwa (13:7), atarudi tena kwenye mlima wa Mizeituni (14:4) na atatawala miaka elfu akiwa mfalme na kuhani mkuu (14:9).
Yaliyomo:
1. Wito wa kumrudia Mungu, Sura 1:1-6
2. Maono manane ya Zekaria, Sura 1:7—6:8
3. Kutangazwa kwa Yoshua, Sura 6:9-15
4. Suala la kufunga, Sura 7—8
5. Hukumu na ukombozi, Sura 9—13
6. Unabii juu ya Masihi, Sura 14

Iliyochaguliwa sasa

Zekaria UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia