Ruthu 3:10-13
Ruthu 3:10-13 SRUV
Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri. Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema. Tena ni kweli kuwa mimi ni jamaa yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi. Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hadi asubuhi.