Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi UTANGULIZI

UTANGULIZI
Waraka huu ni mmojawapo wa Nyaraka za Paulo. Kati ya Nyaraka zote za Paulo huu ni mrefu kuliko zote na wenye mambo mazito kuliko zote. Paulo aliuandika waraka huu katika ziara yake ya tatu ya kuhubiri Injili kule Korintho nyumbani kwa Gayo (16:23; 1 Kor 1:14). Wakati akikaribia mwisho wa ziara yake akipanga kwenda Yerusalemu ili kupeleka michango iliyotoka kwa wakristo wa mataifa (15:25-27), alituma waraka huu Rumi, makao makuu ya dola la Kirumi. Ulipelekwa na mama mmoja aitwaye Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea, bandari ya Korintho (16:1), ambaye wakati huo alikuwa anasafiri kwenda Rumi.
Kanisa la Rumi lilikuwa na waumini wengi waliotoka sehemu mbalimbali (Mdo 2:10), Wayahudi na Wamataifa. Paulo alikuwa bado hajafika Rumi (1:3; 15:22-23). Anajitambulisha kwao na kueleza madhumuni ya ziara yake kwao baada ya kutoka Yerusalemu. Pia anaomba msaada wa kusafirishwa ili kutoka hapo aweze kueneza Injili huko Hispania (1:10-12; 15:20; 24-29).
Ijapokuwa Wayahudi waliwahi kufukuzwa kutoka Rumi (Mdo 18:2) wakati Paulo anaandika waraka huu walikuwa wamekwisha rudi Rumi. Paulo anaona umuhimu wa kuwahubiria Injili Wayahudi na wasio Wayahudi ili waishi kwa amani na kuvumiliana (14:1—15:6). Injili ni kwa ajili ya watu wote wa hali zote (tazama hasa matumizi ya mara nyingi ya “wote” na “kila mtu” – 1:16; 3:9,19,23-24; 4:11,16; 5:12,18). Injili ni “uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (1:16-17). Miongoni mwa mafundisho ya kimsingi anayotupa Paulo ni kwamba watu wote wamefanya dhambi, wako chini ya nguvu ya dhambi, na hukumu ya Mungu iko juu yao (1:18—2:11; 3:19, rejea Gal 3:1,10-11; 5:16-21), torati haiwezi kumwokoa mwenye dhambi (Rum 2:12-29; 3:19-20; 7:1-25, rejea Gal 2:15-16; 3:11-13,21-26), neema ya Mungu iliyofunuliwa katika Kristo (Rum 1:16-17; 3:21-26, rejea Gal 2:20-21; 4:4-7), kuhesabiwa haki kwa imani (Rum 3:26-30; 4:1-5,11, rejea Gal 2:16; 3:11,22-26; 5:1-6) na matunda ya kiroho (Rum 8:1-30, rejea Gal 5:22-26).

Iliyochaguliwa sasa

Warumi UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha