Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi 16:17-24

Warumi 16:17-24 SRUV

Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. Maana utii wenu umewafikia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wasio na hatia katika mambo mabaya. Naye Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.] Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu. Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana. Gayo, mwenyeji wangu, na wa kanisa lote pia, awasalimu. Erasto, wakili wa mji, na Kwarto, ndugu yetu, wanawasalimu. [ Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.]

Soma Warumi 16

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Warumi 16:17-24