Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 8

8
Mhuri wa saba na chetezo cha dhahabu
1 # Zek 2:13; Hab 2:20 Na Mwana-kondoo alipofungua mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa kama nusu saa. 2#Mt 24:31 Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. 3#Amo 9:1; Kut 30:1,3; Ufu 5:8 Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4#Zab 141:2 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. 5#Law 16:12; Eze 10:2; Kut 19:16; Ufu 11:19; 16:18 Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.
Tarumbeta Saba
6Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajiweka tayari ili wazipige.
7 # Kut 9:23-25; Eze 38:22; Yoe 2:30 Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyochangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.
8 # Yer 51:25; Kut 7:20,21 Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. 9Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya meli zikaharibiwa.
10 # Isa 14:12; Dan 8:10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. 11#Yer 9:14 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalifanywa kuwa machungu.
12 # Isa 13:10; Eze 32:7; Yoe 2:10,31; 3:15; Ufu 6:12; Kut 10:21 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, na usiku vivyo hivyo.
13 # Ufu 9:12; 11:14 Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti za baragumu ziliobakia za malaika watatu, walio tayari kupiga.

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo 8: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia