Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 3

3
Ujumbe wa Sardi
1 # Ufu 5:6; 1:16 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. 2#Eze 34:4 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyobakia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. 3#Mt 24:43-44; Lk 12:39-40; Ufu 16:15; 1 The 5:2 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Lakini usipokesha, nitakuja kama mwizi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako. 4#Yud 1:23 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. 5#Kut 32:32-33; Zab 69:28; Ufu 4:4; 6:11; 7:9; 20:12; Flp 4:3; Mt 10:32; Lk 12:8 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. 6Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.
Ujumbe kwa Filadelfia
7 # Isa 22:22; Ayu 12:14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. 8#1 Kor 16:9 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. 9#Isa 49:23; 60:14; 43:4; 45:14; 66:23 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10#Ufu 13:10; Ebr 10:36; Lk 21:19; 2 Tim 2:12 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11#Ufu 1:3; 2:5,10 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. 12#Ufu 21:2; 14:1; 22:4; Eze 48:35; Gal 2:9; Isa 62:2; 65:15 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.
Ujumbe kwa Laodikia
14 # Mit 8:22; Zab 89:37; Yn 1:3; Kol 1:15 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 15#Ufu 2:2; Rum 12:11 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17#Hes 12:8; 1 Kor 3:18; 4:8 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18#1 Pet 1:7; Isa 55:1; Ufu 16:15 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19#Mit 3:12; Ebr 12:6; 1 Kor 11:32 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20#Mk 13:14; Yn 14:23; Lk 12:36; 22:29 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21#Mt 19:28 Yeye ashindaye, nitamridhia kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha