Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 11:1-4

Ufunuo 11:1-4 SRUV

Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wanaosujudu humo. Na behewa lililo nje ya hekalu uliache nje wala usilipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili. Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, wakiwa wamevikwa magunia. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.

Soma Ufunuo 11

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ufunuo 11:1-4